Ajali hiyo imetokea katika
kijiji cha Lubambangwe nje kidogo ya mji wa Chato ambapo basi la Sabuni
Express lenye namba za usajili T275 AZG likitokea mji mdogo wa mugaza kuelekea
jijini Mwanza limepata ajali mbaya katika barabara ya buzirayombo kyemirwa baada
ya kugongana na magari mawili ya mizigo aina ya Scania na kusababisha kifo cha
mtu mmoja na wenguine 30 kujeruhiwa vibaya ambapo baadhi ya majeruhi
wamevunjika miguu na mikono huku mama mmoja mwenye watoto watatu aliyenusulika
kifo katika ajali hiyo akikatiza safari na kurudi nyumbani kwake.
Akizungumza na Chanzo chetu mganga
mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Chato Dr.Pius Buchukundi amesema kuwa
amepokea majeruhi 31 kati yao mmoja akafariki dunia wakati akitibiwa huku
majeruhi wawili wakizidiwa na kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya rufaa
Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi na kwamba majeruhi 20 wametibiwa na
kuruhusiwa ambapo wagonjwa tisa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya
wilaya ya Chato na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
Chanzo ITV