Wednesday, October 7, 2015

UBAKAJI: Njemba Yanaswa Kwa Ubakaji wa Kadenti ka Shule ya Msingi

Njema moja ambaye jinalake halikuweza kupatikana mara moja, anayejishighulisha na ujenzi wa nyumba, mwishoni mwa wiki alinaswa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mdogo wa kike (10) katika nyumba aliyokuwa akiijenga maeneo ya Kichangani mkoani hapa.
 Mtuhumiwa wa Tukio la Ubakaji akiwa chini ya Ulinzi
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa, alikuwa akienda kununua maziwa mtaa wa pili, ndipo jamaa huyo alipomuita ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kumbaka akiwa amemziba mdomo, kumzuia asipige kelele.

Inadaiwa kuwa baada ya kumaliza kufanya kitendo hicho, mtoto huyo aliendelea na safari yake ya kununua maziwa, lakini aliporejea nyumbani, mama yake aligundua hali isiyo ya kawaida hivyo kumuuliza nini kilimsibu.

“Ndipo huyo binti akamwambia mama yake kuwa alipokuwa akienda kununua maziwa, aliitwa na huyo fundi na kufanyiwa kitendo kibaya, jambo ambalo lilimfanya mama huyo kumchukua mwanaye na kumpeleka polisi, ambako walishauriwa kwenda hospitalini kwanza na huko ikathibitika kuwa kweli alibakwa,” alisema shuhuda huyo.


 
Mtuhumiwa wa Tukio la Ubakaji akiwa chini ya Ulinzi
Baada ya vipimo hivyo, mama na mwanaye walirejea tena polisi ambao baada ya kuelezwa hivyo, waliongozana na watu hao hadi eneo la tukio ambapo walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro ili kusubiri mchakato wa kupelekwa mahakamani.