Friday, November 20, 2015

Auawa na Kaka Yake Baada Ya Kukutwa Akifanya Mapenzi na Nguruwe

 Akiwa amefungwa kamba baada ya kufumaniwa

Kijana Saimon Dustan Mwanjavala ‘Mwachakala’ (15), mkazi wa Kijiji cha Mbwila Kata ya Luana, Wilaya ya Ludewa mkoani hapa, amepoteza maisha kufuatia kupigwa na kaka yake wa tumbo moja baada ya kumfumania katika zizi akila uroda na nguruwe.


Tukio hilo la aina yake lilijiri saa 8 mchana wa Novemba 17, mwaka huu ambapo kaka mtu huyo alimkuta mdogo wake ndani ya zizi hilo akiwa katikati ya starehe na nguruwe.

Habari zinadai kuwa, baada ya kushuhudia kitendo hicho kaka huyo alimshika mdogo wake na kumfunga kamba miguuni na mikono kwa nyuma kisha akaanza kumpiga kwa fimbo mwilini.
Akiwa amevuliwa nguo zote baada ya kufumaniwa

Inaelezwa kuwa, wakati wa kipigo kutoka kwa kaka yake, marehemu alikuwa akijitetea kwa kusema kwamba alilazimika kuingia kwenye banda la nguruwe kwa ajili ya kuondoa hamu ya mapenzi kutokana na kubanwa zaidi bila kupata mwanamke.

Licha ya utetezi huo, kaka mtu alimvua nguo zote mdogo wake na kuendelea kumwadhibu mpaka akapoteza maisha.

“Baada ya kuona mdogo wake amepoteza maisha, kaka mtu alilazimika kuuacha mwili chini, akachukua sumu ya panya na kutoweka kusikojulikana,” alisema shuhuda mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Wilbroad Mtafungwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kwamba hadi sasa jitihada za kumsaka mtuhumiwa zinaendelea.
Kamanda Mtafungwa aliwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi kwani hata kama kijana huyo alikutwa akifanya mapenzi na nguruwe bado hukumu yake haikuwa kifo.