Friday, November 20, 2015

BREAKING NEWS! Mtangazaji Maarufu Wa Habari Nchini Afariki Dunia

Mtangazaji maarufu nchini Tanzania Prince Baina Kamukulu amefariki dunia leo alfajiri.

Kamukulu amefariki dunia katika hospitali ya Kigamboni jijini Dar es salaam  ambapo taarifa za awali zinadai kuwa alianguka akiwa mazoezini kisha kukimbizwa katika hospitali hiyo jana usiku.


Kamukulu aliwahi kuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Afrika Bambataa cha Clouds Fm,pia amewahi kufanya kazi Star Tv na Radio Free Africa
Bw. Prince Baina Kamukulu enzi za uhai wake

Bwana Alitoa Bwana Ametwaa jina Lake Lihimidiwe.