Thursday, November 19, 2015

HATARI: Basi La Abiria Lamiminiwa Risasi

Basi moja lililokuwa likisafiri kutoka mjini Juba kuelekea Kampala Uganda limevamiwa na kufyatuliwa risasi asubuhi ya siku ya Alhamisi.
Kulingana na Mwandishi mmoja katika eneo hilo Philip Thon,kisa hicho kilitokea mwendo wa saa moja katika eneo la Moli yapata kilomita 50 kutoka mji wa mpakani wa Nimule.
Maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini wanajaribu kutafuta idadi kamili ya watu waliojeruhiwa.
Watu wanne waliofariki na wengine wanne waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Juba.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa huenda takriban watu 25 wameuwawa huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.
Chanzo chetu mjini Kampala kimezungumza na kamanda wa polisi wa jimbo la Kaskazini mwa Uganda ,karibu na mpaka na Sudan Kusini.
Amesema kuwa maafisa wake wanakutana na kujadiliana na wenzao wa Uganda ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Amesema kuwa wanajaribu kutafuta njia ya kuwasafirisha waliojeruhiwa katika hospitali ya Lacor huko Gulu nchini Uganda.
Amekadiria kwamba takriban watu 69 walikuwa wakiabiri basi hilo.
Patience kwa sasa anajaribu kuitafuta kampuni ya basi hilo kwa jina Friendship.
Haijabainika ni nani aliyeshambulia lakini baadhi ya waliojeruhiwa ambao walizungumza na waandishi ,wanasema washambuliaji walikuwa wamevalia sare za jeshi la Sudan Kusini na walikuwa wakizungumza lugha ya eneo hilo.
Biashara imenoga kati ya Kampala na Juba ambapo mabasi na malori yanatumia barabara hiyo.
Ni mara ya kwanza kwa basi la abiria linalotumia barabara hiyo kuvamiwa katika kipindi cha siku za hivi karibuni

 CHANZO: BBC