Tuesday, November 17, 2015

Wafanyakazi Wagoma Kushinikiza kuongezewa Mshahara.

Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki jijini Dar es Salaam wamegoma kuingia kazini ili kushinikiza uongozi wa kiwanda hicho kutekeleza madai mbalimbali wanayodai ikiwemo kuongezewa mishahara.

Chanzo chetu kilifika katika kiwanda hicho cha Urafiki cha Urafiki kilichopo eneo la Ubungo jijini na kukuta wafanyakazi hao wakiwa wapo nje baadhi yao wakiimba nyimbo mbalimbali za kudai haki zao na wengine kuomba rais Dakta John Pombe Magufuli kuingilia kati sakata hilo kwani wengi wao wanafanya kazi ngumu kwenye mashine lakini wanaamubulia mishahara kiduchu.
Baadhi ya wazee walionekana kuwa miongoni mwa wafanyakazi hao wamesema uongozi wa kiwanda hicho wameshindwa kutekeleza agizo la mahakama ya usuluhishi ambayo ilisema uongozi wa kiwanda hicho pamoja na chama cha wafanyakazi wakae pamoja ili kupitia majina ya watu wanaotakiwa kulipwa ili zoezi hilo ifanyike lakini mpaka sasa agizo hilo la mahakama imeshindwa kutekelezwa.


Licha ya kiwanda hicho kuwa na wafanyakazi wa raia wa China, kutokana na ubia uliopo kati ya Tanzania na China lakini raia wa China wanadaiwa kukimbia huku mmoja akionekana dirishani juu ya gorofa akipiga picha kwa kujificha, ambapo naibu meneja mkuu msaidizi na meneja utawala Bwana Moses Swai, amekiri wafanyakazi hao kuwa namadai ya muhimu lakini amesema wapo katika hatua za mwisho hivyo akawaomba kuendelea na kazi.
CHANZO: ITV