Wednesday, December 30, 2015

Askari Wawili Wamekufa na Wengine Kujeruhiwa Wakiwa Doria


Askari wawili wa cheo cha koplo jijini Tanga wamekufa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya wakati wakiwa doria baada ya gari lao lililokuwa katika mwendo kasi lilipopatwa na hitilafu kisha kuacha njia na kupinduka.

Akielezea tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga mratibu mwandamizi Too Mayala amesema baada ya gari kupatwa na hitilafu dereva wake alijitahidi lisitumbukie katika daraja la mto neema lililopo katika barabara kuu inayonganisha jiji la Tanga kwenda Pangani ndipo alipokwenda kugonga msingi wa daraja hilo kisha gari kupinduka.
 
Kamanda Too amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Kassim Jumanne aliyekufa papo hapo muda mchache baada ya ajali na othaman kilale ''STRUGLE'' ambaye alikuwa ndio dereva wa gari hilo aliyekuwa amejeruhiwa sehemu za kifuani baada ya kubanwa na usukani wa gari hilo.
 
Amewataja waliojeruhiwa vibaya kuwa ni Martina Pascal na Vitalisi James Ndogo ambao wana cheo cha polisi Constebo.
 
Hata hivyo kamanda Too amesema kulingana na ajali hiyo jeshi la polisi litagharimia matibabu kwa majeruhi kufuatia mmoja kati ya wawili hali yake sio ya kuridhisha sana na anatarajiwa kusafirishwa hospitali ya rufaa ya Muhimbili kwa ajili ya tiba zaidi.

Chanzo: ITV