Wednesday, December 30, 2015

TRA Yatoa Onyo Kwa Kampuni 5 za Simu kwa Kukaidi Kuhakikisha usalama kwenye mitandao yao

Mamlaka ya mawasiliano nchini -TCRA imetoa onyo kali kwa kampuni 5 za simu na kuziagiza zilipe faini ya shilingi milioni 25 kwa kukaidi agizo la mamlaka hiyo la kuhakikisha usalama kwenye mitandano yao.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Profesa Ally Simba amesema wamepokea malalamiko mengi ya watu kutapeliwa ambapo imekuwa ni kawaida kwa wateja wa makampuni hayo kutapeliwa fedha huku makampuni yakiacha kudhibiti vitendo hivyo ingawa uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Chanzo: ITV