Sunday, December 13, 2015

JOB VACANCY: Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi

HALMASHAURI YA WILAYA KILINDI


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI (LINARUDIWA)

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kilindi anaeatangazia wananchi kuomba kujaza nafasi za kazi zifuatazo:

1. Katibu Mahsusi III Nafasi 2
Ngazi ya Mshahara TGS B

Sifa za Mwombaji
• Awe amehitimu kidato cha nne na kuhudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu.
• Awe amefaulu somo la hati/Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.
• Awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na kupata cheti katika program za windows Microsoft Office, Internet, E-mail na publisher.

Kazi na Majukumu
• Kuchapa barua taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni, kuwasaidia shida zao na kuwaeleza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za kvikao.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaisizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia
• Umri kila mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 ya kuzaliwa.
• Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika mazingira ya vijijini na si chini ya miaka mitatu baada ya kuajiriwa.
• Barua zote za maombi ziandaliwe kwa mkono na mwombaji mwenyewe na ziambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma na ujuzi. Pia mwombaji alete picha mbili (2) za passpoti na cheti cha kuzaliwa.
• Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18/12/2015 saa 9:30 alasiri.
• Maombi yote yatumwe kwa

Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P 18
SONGE-KILINDI

Source: Mwananchi 5th December, 2015