Saturday, December 12, 2015

NEWS: Polisi Nachini Tanzania Imetangaza Zawadi Nono ya Takribani Dola elfu 10 kwa atakayesaidia kupatikana kwa mshukiwa wa Sakata Bandarini

Kontena
Polisi nchini Tanzania wameahidi zawadi kwa atakayesaidia kukamatwa kwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni moja anayetuhumiwa kuhusika katika kupitisha makontena bandarini bila kulipiwa kodi.
Kamanda kamishna wa polisi Suleiman Kova amesema wanamtafuta Abdulkadir Kassim Abdi, 38, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Regional Cargo Services LTD.
Anashukiwa kuhusika katika kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya Azam (Azam ICD) bila kulipia kodi.
Abdulkadir ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni zilitumiwa kutoa makontena hayo bandarini, kwa mujibu wa serikali.
Polisi imetangaza zawadi nono ya takribani dola elfu 10 kwa atakayesaidia kupatikana kwa mtuhumiwa.
Makontena hayo 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya Azam kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015.
Uchunguzi wa awali ulikuwa umeonyesha makontena 2489 yalitolewa Bandari ya Dar es Salaam kati ya Machi na Septemba 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.