Thursday, December 17, 2015

NEWS: Wachina Nchini Watupwa Jela Miaka 20

Kuhusu faini kwa kosa hilo, Hakimu Mkazi Michael Mteite amesema Wachina hao wanatakiwa kulipa mara kumi ya thamani ya pembe za faru walizokutwa nazo ambacho ni kiasi cha sh9bilioni.

Hata hivyo, wakili wa washtakiwa hao, Ladislaus Rweikaza amesema kuwa ataisoma nakala ya hukumu hiyo na kisha kujadiliana na wateja wake ili kujua iwapo watakata rufaa ama la. Hata hivyo, mwanasheria huyo amesema kuwa hukumu kwa wateja wake haimaanishi kuwa imetolewa kwa misingi ya ubaguzi bali inatokana na kosa walilokutwa nao raia hao.

Chanzo: Mwananchi