Thursday, January 28, 2016

Kivuko Chenye Watu 30 Chazama Kilombero

Watu wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi, kufanya kigonge nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji.
Tukio la kivuko hicho cha mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza
Chanzo: ITV