Thursday, February 11, 2016

AJALI MBAYA: Watu 11 wafariki dunia 29 wajeruhiwa katika ajali ya Simba Mtoto na Lori Muheza Mkoani Tanga

Watu 11 wamekufa papo hapo na wengine 29 wamejeruhiwa na watano kati yao hali zao ni mbaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni ya Simba Mtoto kugonana na lori la mchanga Muheza Mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,MIHAYO NSIKELA  ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Pangamlima,Kata ya Bwembera Wilayani Muheza wakati dereva wa lori, ambaye yeye na mwenzake wa Simba Mtoto wamekufa alipokuwa akilkwepa gari dogo ndipo alipokutana na basi.
Basi hilo lilikuwa likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam na lori lilikuwa likitokea Mkoani Kilimanjaro.
Amesema baadhi ya miili imehifadhiwa kayika Hospitali teule Wilayani Muheza kwa ajili kutambuliwa na majeruhi wanaendelea na matibabu na wenye hali mbaya wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Rufaa ya Mmoa wa Tanga - Bombo.

Kamanda NSIKELA amsema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.