Saturday, April 2, 2016

Arsenal,Chelsea na Man City zapata ushindi mkubwa


Arsenal imeimarisha matumaini yao ya kuwania taji la ligi ya Uingereza mwaka huu baada ya ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Watford.
The Gunners walichukua uongozi baada ya dakika nne za kipindi cha kwanza baada ya Alexi Sanchez kufunga bao la kwanza kupitia pasi nzuri ya Iwobi.
Iwobi baadaye alifunga bao la pili,Bellerin la tatu kabla ya Theo Walcot kufanya mambo kuwa 4-0 baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada.
Alexandre Pato aliifungia Chelsea bao lake la kwanza dhidi ya Aston Villa huku matumaini ya timu hiyo kusalia katika ligi hiyo yakididimizwa baada ya kufungwa mabao 4-0.
Mashabiki wa Aston Villa waliimba nyimbo dhidi ya mmiliki wa kilabu hiyo randy Lerner huku The bLues ikitawala mechi hiyo kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.
Matokeo mengine:
Bournemouth 0 Man City 4
Norwich 3 Newcastle 2
Stoke 2 Swansea 2
Sunderland 0 West Brom 0