Friday, April 15, 2016

Jeshi la polisi Kigoma linamshikilia Mganga wa zahanati kwa tuhuma za kubaka mgonjwa

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Mganga wa Zahanati ya kijiji cha Kidahwe wilayani Kigoma kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekuwa akimtibu katika zahanati ya kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ferdinand Mtui amemtaja mganga huyo kuwa ni Ibrahim Bundala (29)na kwamba anatuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 aliyefika katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupata matibabu.
 
Amesema mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika alitenda kosa hilo baada ya binti huyo kuingia katika chumba cha daktari kwa ajili ya kumueleza ugonjwa anaoumwa.