Thursday, April 7, 2016

Mwanafunzi wa kiume anayepata ''hedhi''


George Fellowes ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamni kwamba hata yeye hupatwa na ''hedhi ya kiume''.
Anasema kuwa ni rafiki wa karibu wa Amber May Ellis jirani yake na hivyobasi hupata uchungu wa hedhi kila mwezi rafikiye anapopata hedhi.
Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa.Akizungumza na Newsbeat,George anaelezea:Nadhani ni swala la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile za wanawake.
Ninapata uchungu chini ya tumbo langu pamoja na katika kinena.Huwa nahisi vibaya na kuwa na hasira na marafiki wangu wengi.Pia huwa na hisia zenye mhemuko.
''Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi.Kuna kitu kimoja kisichomuathiri George hatahivyo.
Sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu'',anasema.
''Wakati unapokuwa rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana''.
George anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliopita alitaka ushauri wa daktari wake.
Lakini hakukuwa na maelezo hivyobasi alipewa dawa za kumaliza maumivu ya kinena.
Chanzo: BBC