Monday, May 30, 2016

Aliyemchinja mwanamke Dar ashikiliwa na Polisi

Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikiria mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Anneth Msuya aliyeuawa kwa kuchinjwa hivi karibuni, Kigamboni wilaya ya Temeke jijini Dar es alaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa wanamshikilia mtu huyo kwa uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya mwanamke huyo.
 
Aidha  polisi  imefanikiwa kuwauwa majambazi wawili waliokuwa wamevamia mtu na kunyanganya  begi lenye fedha  katika eneo la Mburahati ambapo polisi walipamba nao  kwa kushirikina na wananchi ambapo majambazi hayo yalikimbilia Kisukuru na  baada ya mabishano makali yaliuawa.