Wakizungumza katika eneo la tukio baadhi ya waathirika ambao ndugu
jamaa na zao wamechinjwa majira ya saa saba usiku wamesema kundi la
watuhumiwa wanaokadiriwa kuwa walikuwa watu nane na kuvalia nguo nyeusi
walipofika katika nyumba zao waliwaamuru akina baba watoke nje kisha
kuwapeleka hadi katika vichaka kisha kuwachinja.
Tukio hilo limekuja wiki mbili tu baada ya vikundi hivyo vya
uhalifu vinavyodaiwa kujificha katika mapango ya Amboni Mleni Maji moto
kuchinja mbuzi 48,ng'ombe wawili na kuku zaidi ya 12 lakini Kamanda wa
Polisi amekiri kuwa tukio hilo ni kubwa na kwamba jitihada za polisi
zinafanywa ili kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanakamatwa na kutiwa
mbaroni.
Hata hivyo ndugu wa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kibatini ambaye
naye ni miongoni mwa waliochinjwa amesema chanzo cha kundi hilo
kuwafanyia unyama huo inatokana na kukamatwa kwa watoto wa watuhumiwa
ambao ndio waliokuwa wakitumwa kabla makundi hayo hayafanya uhalifu.
Chanzo ITV