Saturday, August 6, 2016

Baba na Mtoto Wauawa kikatili shambani



Kigoma. Watu wasiofahamika wamewaua baba na mtoto waliofahamika kwa jina la Haruna Katutu na Sarehe Haruna na kumjeruhi mama wa familia hiyo katika mashamba ya Lulengela yaliyopo Kijiji cha Shunga wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Uzia Ruhasha alisema taarifa za tukio hilo alizipata asubuhi baada ya wapita njia kuwaona wakiwa wamelala shambani walipowasogelea walibaini kuwa walikuwa wameshafariki dunia.
Alisema walitoa taarifa polisi lakini walifika saa kumi na moja jioni kuichukua miili hiyo kwa uchunguzi zaidi.
“Tumesikitika kuona vifo vya watu wasiokuwa na hatia kijijini hapa, lakini tunashangaa tangu Saa 1:00 asubuhi tulipotoa taarifa polisi, walifika saa 11:00 jioni walikuwa hawajawasiri eneo la tukio kufanya uchunguzi,” alisema Ruhasha.
Chanzo: Mwananchi

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>