Saturday, August 6, 2016

M’kiti mbaroni kwa kumdakisha mimba mwanafunzi

Mwanza. Polisi mkoani Mwanza wanamshikilia mwenyekiti wa Mtaa wa Sangabuye, Kata ya Igombe Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, John Shija (38) kwa madai ya kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili (Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 14.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema alikamatwa Agosti 3, saa 9:30 alasiri.
Alidai kuwa mtuhumiwa alimtorosha na kumpa ujauzito mwanafunzi huyo anayesoma Shule ya Sekondari Sangabuye.
Pia, polisi inamshikilia mama mzazi wa mwanafunzi huyo kwa kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa polisi alipokuwa akihojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Chanzo: Mwananchi

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>