Thursday, December 29, 2016

Mzee wa miaka 75 alala nje kwa miaka minne baada ya nyumba yake kudondoka.

Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania UWT,ya Chama cha Mapinduzi CCM -katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imelazimika kumjengea nyumba Bibi Rukia Salehe mwenye umri wa miaka zaidi ya 75 ambaye amekuwa akilala nje kwa miaka minne mfululizo licha ya juhudi zake za kuomba msaada kwa mamlaka husika kushindikana.

Akizungumza kwa masikitiko bibi rukia salehe anasema nyumba aliyokuwa akiishi hapo awali ilianguka baada ya kuwa na nyufa nyingi,hivyo kukosa uwezo wa kujenga nyumba nyingine,huku akisisitiza katika maisha yake hajawai kupata mtoto licha ya kutumia muda mwingi kulea watoto wa ndugu na marafiki lakini wameshindwa kumsaidia.

Akimzungumzia  bibi huyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Matopeni Omar Hussein anasema licha ya  bibi huyo kuomba msaada ofisi ya mkuu wa wilaya lakini amegonga mwamba,hali iliyolazimu  diwani wa Chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na wanachama wa UWT kumsaidia ili kumuondoa katika mazingira hatarishi.

Kibanda cha bibi Rukia anachoishi ni hatarishi lakini amekuwa akikitumia kulala kuhifadhi vitu vyake na kupikia huku mvua jua likimuwakia kutwa kucha.