Wednesday, January 11, 2017

Wadaiwa wajinyonga kutokana na msongo wa mawazo




Tabora. Wanawake wawili wamefariki dunia kwa kujinyonga katika matukio mawili yaliyotokea mikoa ya Geita na Tabora yanayohusishwa na msongo wa mawazo.
Wakazi hao ni Mwajuma Hamad, Mkazi wa Miyogoni, Manispaa ya Tabora, ambaye alijinyonga chumbani kwa kile kinachodaiwa ni kuchukizwa na kitendo cha mume wake, Juma Kiligito kumzuia kujihusisha na ujasiriamali wa ushonaji nguo, huku mwenzake Anastazia Kahezi (65), mkazi wa Kijiji cha Nyarututu Wilaya ya Chato mkoani Geita alijinyonga kwa kusongwa na mawazo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi, huku Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiwaomba wenye taarifa kujitokeza kusaidia upelelezi
 Chanzo:MWANANCHI

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>