Tuesday, May 16, 2017

Amnyonga mtoto wake siku tatu baada ya kujifungua

POLISI mkoani Kagera linamshikilia binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Latifa Vedasto (18) mkazi wa mtaa wa Ntungamano kata ya Buhembe Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaa kwa kumnyonga.
Tukio hilo ambalo limewashtua wakazi wa mtaa huo baada ya kupata taarifa ya binti huyo kudaiwa kumnyonga mtoto wake aliyejifungua siku tatu zilizopita.
Baada ya kutekeleza unyama huo binti huyo alimzika kichanga huyo bila kumjulisha mtu yoyote, jambo ambalo lilifanya majirani zake kumtilia mashaka na kuita polisi kumkamata na polisi kufukua sehemu hiyo aliyomfukia na kukuta kichanga hicho kikiwa kimepoteza maisha.
Hata hivyo nchini Tanzania tatizo la mimba za utotoni nchini limeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia 27% mwaka 2016/17, kutokana na ukosefu wa huduma pamoja na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19 linalopelekea kuongezeka kwa mtukio kama haya.
Chanzo: Mwananchi

 MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA 

AJIRA MPYA ZIMETANGWAZWA, BOFYA HAPA
http://studentswagas.blogspot.com/