Saturday, May 6, 2017

BREAKING NEWS: Wanafunzi zaidi ya 20 wafariki katika ajali ya basi Karatu

Wanafunzi zaidi ya 20 wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya basi iliyotokea wilayani karatu leo asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, basi hilo aina ya Mitsubish Rosa lilikuwa limewabeba wanafunzi likitokea Arusha mjini na kupata ajali hiyo katika wilaya ya Karatu.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Therezia Mahingo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Chanzo halisi cha ajali hiyo bado hakijafahamika hadi sasa. Tutaendeleea kuwajuza kuhusu tukio hili.





"INALILLAHI WAINA ILLAIHI RAJIUN, BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE"