Wednesday, May 17, 2017

KUOSHA SANA UKE KUNASABABISHA HARUFU MBAYA

Watu wengi wanaamini kuwa kuosha sana sehemu za siri kunasaidia kuondoa harufu mbaya kwa wanawake. Ndio Uchafu husababisha harufu mbaya, lakini Kuosha sana uke nako pia ni tatizo.

Tatizo la kutoka harufu mbaya ukeni husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. 
Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.
Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya.
Haimaanishi kuwa wanawake waache kujisafisha lakini kujisafisha kwa kupindukia kunaweza kuleta tatizo kuongezeka zaidi.