Wednesday, May 17, 2017

Njemba Yamkata Kiganja Mpenzi wake Mwanza

POLISI mkoani Mwanza inamshikilia mtu mmoja nayejulikana kwa jina la Mkama Mgengele (36), mkazi wa kisiwa cha Ghana katika Kijiji cha Kamasi Kata Ilangala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, kwa tuhuma za kumfanyia ukatili mtu anayedaiwa kuwa mpenzi wake kwa kumkata kiganja cha mkono wake wa kushoto

Mgengele anadaiwa kufanya tukio hilo la kumkata na kitu chenye ncha kali kwenye kiganja cha mkono wa kushoto hadi kudondoka chini mpnzi wake huyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, alisema Mei 14 mwaka huu majira ya usiku, mtuhumiwa alimkata kiganja cha mkono wa kushoto kisha akamkata tena kwenye paja la mguu wa kulia, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Ester Lazalo (37)ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake.
Msangi alikuwa hivi karibuni walikuwa katika mgogoro wa kimapenzi na kwamba mtuhumiwa alifika kazini kwa Ester na kuanza kumrushia maneno makali kabla ya kumkata
Chanzo: Nipashe

Matukio zaidi ya Kusisimua Bofya hapa