Wednesday, May 31, 2017

Watafiti: Uendeshaji boda boda ni hatari kwa uzazi

Vijana wengi Afrika Mashariki wamekuwa wakitumia baiskeli kufanya biashara ya uchukuzi wa abiria, maarufu kama boda boda.
Ni kazi inayohitaji mhudumu atumie nguvu nyingi za mwili wake.
Sasa, watafiti nchini Kenya wanasema kunaweza kuwa na changamoto nyingine - kwamba wahudumu wa bodaboda wanakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wao wa uzazi. 
Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba waendeshaji boda boda walikuwa katika hatari ya kutoweza kutanua mishipa ya damu kwenye uume wakati wa kushiriki tendo la ngono.
Mmoja wa watafiti hao Isaac Wamalwa ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta aliambia BBC kwamba suluhu huenda likawa ni kutumiwa kwa kiti maalum ya waendesha baiskeli ambayo hakitadhuru uume wa waendeshaji.
Bw Wamalwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi alifanya utafiti miongoni mwa vijana eneo la Bungoma, magharibi mwa Kenya.
Walichunguza wahudumu 115 wa boda boda wa umri wa chini ya miaka 40 eneo hilo, wakishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.
Anatahadharisha pia kwamba maelfu ya vijana wanaofanya mazoezi kwenye vituo vya mazoezi mijini, kwa Kiingereza gym, ambapo huendesha baiskeli zisizosonga, wanakabiliwa na hatari sawa na hiyo.
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC

Habari nyingine:

http://studentswagas.blogspot.com/