Wednesday, October 14, 2015

Chadema Yaaswa Kuachia Majimbo na Viongozi wao. HABARI KAMILI BOFYA HAPA=>

Mgombea mwenza wa urais kwa tiketu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Juma Duni Haji amewataka wagombea ubunge katika majimbo ya Buyungu Na Kasulu Mjini Mkoani Kigoma kuheshimu  uamuzi w a viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi - UKAWA  wa kuachiana majimbo ili kuepuka kugawana kura na hivyo kutoa mwanya kwa Chama cha Mapinduzi kuendelea kushinda katika uchaguzi mkuu wa  tarehe   25  mwezi huu .
Katika jimbo la Buyungu Wilayani Kakonko ambako mgombea mwenza wa Urais , JUMA DUNI HAJI amefika kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kuziguzigu na kujikuta akishindwa kumnadi mgombea ubunge wa chama cha NCCR Mageuzi,MAWAZO ATHANAS METHUSELA baada ya wananchi kudai kuwa mgombea anayekubalika katika jimbo hilo ni wa CHADEMA  Mwalimu KAFUKU BULAGO .
 Mgombea mwenza wa urais kwa tiketu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Juma Duni Haji
Katika jimbo la Kasulu Mjini nako hali si shwari baada ya wagombea watatu wa vyama vinavyounda UKAWA kujitokeza kwa pamoja kuwania kinyang'anyiro cha ubunge katika jimbo hilo ambalo lilikuwa linaongozwa na MOSES MACHALI wa NCCR Mageuzi kabla ya kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.


Licha ya migogoro hiyo, mgombea mwenza huyo wa urais amefanya mkutano mwingine katika uwanja wa taifa jimbo la Muhambwe,mjini Kibondo na kuahidi kuwa iwapo wananchi watamchagua EDWARD LOWASSA kuingia ikulu, atahakikisha anaijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Nyakanazi hadi Kidahwe.
Chanzo ITV
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA=>