Sunday, October 25, 2015

Gari La Kampeni Meneja Lashambuliwa Vibaya na Wananchi

Gari la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea Ubunge jimbo la Moshi vijijini kwa tiketi ya CCM Dk. Cyrill Chami, limeshambuliwa na kuharibiwa vibaya na wananchi wakilishuku kuwa na kura bandia.

Katika tukio hilo lililotokea leo majira ya saa 10:00 Alasili katika kijiji cha Uhuru kitandu, Meneja wa Kampeni huyo aitwae George kitandu aliokolewa na Polisi lakini kwa wakati hio akiwa amejeruhiwa vibaya.

Gari hilo aina ya Toyota Verosa namba T 750 CPB liliharibiwa vibaya kwa kuvunjwa vunjwa vioo, Kung'olewa magurudumu yake, kuibiwa redio ya gari na vifaa mbalimbali.
Chanzo Mwananchi: