Monday, October 26, 2015


Hujambo? karibu katika matangazo ya DIRA YA DUNIA REDIO, yafuatayo ni muktasari wa yale tuliyokuandalia.
Matokeo ya uchaguzi yaendelea kutangazwa nchini Tanzania huku ushindani mkali ukiwa baina ya chama tawala CCM, na vyama vinavyounda Muungano wa UKAWA.
Wakati hayo yakijiri vurugu zaripotiwa visiwani Zanzibar baada ya mgombea urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kujitangaza kuwa ameshinda.
Nacho chama tawala CCM chajitangaza kupata ushindi kwenye majimbo ya Tanzania.
Nacho chama cha Mapinduzi kwa upande wake nacho kimejitangaza kuwa kimepata ushindi katika majimbo majimbo 176
Ungana Nasi tukuhabarishe mengi na ushee ,bila kusahau matangazo maalumu ya uchaguzi nchini Tanzania 2015.
KARIBU