Sunday, October 4, 2015

MAUAJI: Mama na Mtoto Wauawa Kwa Kukatwa na Mapanga. HABARI KAMILI BOFYA HAPA=>

Mkazi wa kijiji cha Sharangula kata ya Nyamwilolela mkoani Geita na Mwanawe wameuawa kwa kukatwa na mapanga na watu ambao hawajajulikana.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati mwanamke huyo mageni Hongera (25) akiwa amembeba mgongoni mwanae Joyce Ndarusanze (1) akitokeakwenye kibanda chake cha biashara kuelekea nyumbani kwake.

Kaimu kamanda mkoa wa Geita, Peter Kakamba alisema jana kuwa askari wa jeshi hilo wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha mauaji hayo.

"Ni kweli tukio limetokea, lakini bado sijakusanya vizuri taarifa zake) alisema Kakamba.

Mwenyekiti wa kijiji hiko cha Sharangula, Yuda Nghindi alisema kuwa mwanamke huyo alikatwa sehemu za shingoni na mtoto wake alikatwa kichwani.

Alisema kuwa mwanamke huyo alikuwa na kibanda cha biashara kijijini hapo na alifikwa na mkasa huo umbali wa mita kumi kutokea nyumbani kwake.

Alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana na uongozi wa kijiji unafuatilia kwa kina kuweza kubaini wahusika wa mauaji hayo.
Chanzo: Mwananchi

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA=>