Tuesday, March 15, 2016

Mertesacker Awatolea Uvivu Washambuliaji Wa Arsenal

Beki wa Arsenal Per Mertesacker ameshusha lawama kwa timu yake na kusema kuwa matokeo mabovu yanayowakabili hivi sasa yanatokana na kukosa umakini langoni mwa timu pinzani.
Mwishoni mwa wiki, Arsenal walitupwa nje ya kombe la FA baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Watford katika dimba la Emitares, huku Danny Welbeck ambaye aliifungia Arsenal goli pekee akikosa goli la wazi katika dakika za lala salama.
Mbali na kipigo cha Watford, Arsenal pia walifungwa na Swansea, Manchester United na Barcelona, hivyo Mertesacker analia juu ya safu yao ya ushambuliaji kukosa umakini.
“Tunachokosa kwa sasa ni suala la umaliziaji. Inonekana kana kwamba tunacheza tu halafu hatufungi badala yake tunafungwa sisi”, Mertesacker alisema.