Friday, August 5, 2016

UKATILI: Mtoto anajisiwa

Kigoma. Mtoto wa miaka mitano amelawitiwa karibu na kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo Msufini, Mwanga mjini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema mtoto huyo alipotea wakati mama yake Genovete Rafael ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo katika Soko la Msufini lililopo Mwanga akiwa katika biashara zake.
Amedai kuwa mtoto huyo alimtoroka mama yake na kwenda kusikojulikana, ndipo watu walianza kumtafuta kwa kusaidiana na mzazi wake huyo.
Kamanda Mtui amesema ilipofika saa tatu usiku walifanikiwa kumkuta mtoto huyo akiwa jirani na kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo pembeni kidogo ya soko la Msufi.

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>