Tuesday, May 30, 2017

Mzee anayedaiwa kuchora nembo ya taifa afariki Muhimbili

Dar es Salaam. Msanii anayedaiwa kuchora nembo ya Adam na Hawa, iliyotumika kitaifa, Francis Maige (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Ngosha aliyepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita kwa ajili ya matibabu, amefariki dunia saa 2 usiku Mei 29.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili imeeleza kuwa hali ya Ngosha ilibadilika ghafla akiwa hospitali hapo.
“Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hapa Muhimbili na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na mamlaka husika.” imesema taarifa hiyo.

 MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA 

AJIRA MPYA ZIMETANGWAZWA, BOFYA HAPA
http://studentswagas.blogspot.com/