Mama aliyekuwa amewaalika watoto katika sherehe ya kuzaliwa kwa mwanawe amejikuta katika wakati mgumu sana kufuatia na vifo vya watoto watatu waliofariki siku ya jumapili wakiwa katika sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa mtoto mwenzao aliyetimiza mwaka mmoja. Tukio hilo lilitokea juzi jioni katika Hoteli ya Landmark, Kunduchi Beach Dar es Salaam ambapo watoto hao walifariki duni baada ya kutumbukia kwenye Swimming-pool siku hiyo.
Waliofariki katika ajali hiyo ni Ndimbumi Sisala (9), mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Kijitonyama, Janeth Kihoko (9) wa darasa la nne Shule ya Msingi Dk Omar Ali Juma na Eva Mwakatobe (11) aliyekuwa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Shekilango.
Mwanamke huyo aliyekuwa amewaalika watoto hao anaonekana kuwa katika wakati mgumu zaidi kuliko hata wafiwa. na mbaya zaidi ni kitendo cha mzazi wa mtoto mmoja kuipokea kwa kinyongo hali hiyo huku wazazi wengine wakimshukuru mungu na kuamini kuwa yote ni mipango ya Mungu.