Mwingine anusurika kifo baada ya jaribio la kuporwa pikipiki na majambazi kushindikana.


Tanga. Mkazi wa Kijiji cha Duga Horohoro Tanga, Mbito Dilima amejiua kwa kujinyoga akitumia chandarua na kuacha ujumbe kuwa, sababu ya uamuzi huo ni kulazimishwa kuoa mwanamke asiye chaguo lake.


Kaimu kamanda wa polisi wa mkoani Tanga, Juma Ndaki alisema mtu huyo alijinyonga akiwa chumbani kwake juzi saa 2:00 usiku.


Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa, marehemu alichukua uamuzi wa kusitisha uhai wake kutokana na wazazi wake kumlazimisha kwa muda mrefu kumuoa binti ambaye hakumpenda, hivyo kuibua mzozo wa kifamilia.


Ndaki alisema karatasi iliyoandikwa ujumbe huo aliiweka sikioni kama msokoto wa sigala na kwamba wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na ukweli wa ujumbe aliouacha marehemu.


“Uchunguzi wetu, kwanza ni kuwahoji wazazi wa marehemu na kupata ushahidi mwingine kutoka kwa majirani kama utakuwapo,” alisema Ndaki.


Katika tukio jingine, Ndaki alisema kuwa dereva wa bodaboda, Juma Said alinusurika kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi. Endelea>>


 
Top