Magazeti nchini India yameripoti kisa cha kutamausha kilichotokea katika ndege ya shirika la Air India.
Abiria
 mmoja aliyekuwa safarini kuelekea mjini London Uingereza akitumia ndege
 ya shirika la ndege ya Air India alizua hofu miongoni mwa abiria 
wengine alipopiga kamsa kwa mshtuko baada ya kumpata mjusi kafiri ndani 
ya mlo wake.
Abiria wote walitamauka wasijue kilichompata mwenzao 
haswa wakati huu ambapo kunataharuki kubwa na tahadhari  kuhusiana na 
maswala ya usalama kufuatia matukio ya ugaidi kote duniani.
Mjusi kwenye mkate  
Bwana
 huyo ambaye awali alikuwa ameagiza chakula maalum kutoka kwa mhudumu wa
 ndege  hakuamini macho yake alipokaribia kumla mjusi macho makavu !
Inasemekana kuwa alipofungua  mkate wake akitaka kuunga'ta mara akaona ukitikisika. Ghafla bin vu  akaona mjusi akijifurukuta akitafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye plastiki iliyokuwa imefunika chakula chake. 
Alipiga mayowe kwa sauti ya juu usingeliamini kuwa ni mwanaume.
Shirika
 hilo limekanusha habari hiyo japo kuna picha inayoendelea kusambazwa 
katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikionesha mjusi mdogo 
kwenye mkate.
Waziri wa usafiri wa anga ametao onyo kwa shirika hilo akisema kuwa halifai kuwapakulia wateja wake mijusi!
 Chanzo: BBC

