Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 – 05 Juni 2016.
Vijana waliochaguliwa, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za michezo kama vile ‘track suit’, bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa kwenye makambi yenye baridi kama JKT Makutupora, JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT Mtabila.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, uhodari, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 20 Mei 2016

****

MAJINA YA WANAFUNZI KIDATO CHA 6 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT KATIKA KAMBIMBALIMBALI NCHINI 2016

1. JKT Rwamkoma - Mara

2.  JKT Mafinga - Iringa

3.  JKT Kambi ya Makutopora - Dodoma

4. JKT Mtabila - Kigoma

5. JKT Kanembwa - Kigoma 

6. JKT Bulombora - Kigoma

7.  JKT Ruvu - Pwani

8. JKT Mgambo - Tanga

9.  JKT Maramba-Tanga

10. JKT Mlale- Songea

 11. JKT Msange -Tabora

 
Top