Wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili na wanaume wanaofanya
mapenzi ya jinsia moja sasa wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi
vya Ukimwi aina ya Truvada kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo
badala ya kutumia mipira ya kondomu. Picha na Maktaba
Kwa ufupi
Mwananchi lilizungumza na baadhi ya wafanyabiashara
ya ngono jijini katika maeneo ya Mwananyamala Hospitali, Komakoma na
Vingunguti ambao walisema kuwa wanatumia dawa hizo kwa ajili ya kuzuia
maambukizi ya VVU ili kuwaridhisha wateja wasiopendelea mipira hiyo.
Habari Kamili
Dar es Salaam. Wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili na wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja sasa wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi aina ya Truvada kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo badala ya kutumia mipira ya kondomu.
Dar es Salaam. Wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili na wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja sasa wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi aina ya Truvada kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo badala ya kutumia mipira ya kondomu.
Mwananchi lilizungumza na baadhi ya
wafanyabiashara ya ngono jijini katika maeneo ya Mwananyamala Hospitali,
Komakoma na Vingunguti ambao walisema kuwa wanatumia dawa hizo kwa
ajili ya kuzuia maambukizi ya VVU ili kuwaridhisha wateja wasiopendelea
mipira hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara hao walidai kuwa
wanatumia Truvada kuzuia maambukizi pindi wanapokutana na wanaume
wakware ambao huwabaka au kuwalazimisha kufanya mapenzi bila kinga.
“Hizi dawa tunazipata katika hospitali na wakati
mwingine katika maduka makubwa ya dawa. Kwa sababu zinazuia maambukizi
ya Ukimwi na sisi ni watu ambao tunafanya kazi katika mazingira
hatarishi,” anasema Leyla Musa, mmoja wa wanawake hao.
Si hivyo tu, kwa kuwa hii ni biashara baadhi yao
hukubali kufanya mapenzi bila mipira ili kupata fedha nyingi kutoka kwa
wanaume.
Wengine hukimbilia huduma ya PEP
Baadhi ya wanawake hao wanasema kuwa baada ya
kufanya mapenzi na wanaume kadhaa asubuhi huenda katika kliniki
zinazotoa huduma za ARV na kudanganya kuwa wamebakwa na kisha hupewa
huduma za dharura za ARV zinazoitwa kwa kitaalamu Post-exposure
prophylaxis.
Kwa kawaida mtu aliyebakwa au kujikata hupewa dawa aina ya Lamivudine, Zerophidine au Truvada kulingana na uzito wa tatizo.
“Tunatumia hizi dawa mara kwa mara lakini
tunafanya hivyo katika kliniki tofauti ili tusigundulike,” alisema mmoja
wao, mkazi wa Mwananyamala, Mariam Leshaniki.
Kwa maelezo ya Dk Rachel Baggaley, mtaalamu wa
masuala ya Ukimwi wa Shirika la Afya Duniani anasema dawa za PEP zipo
maeneo mengi duniani kwa sasa na zinafanya kazi kwa ufanisi pia hazina
madhara kwa mwanamke.
“Dawa hizi siyo sumu mwilini, zinaingia kwenye
mfumo wako wa damu kabla virusi havijajizatiti na inavizuia ili mradi
uzitumie ndani ya saa 72,” anasema Dk Baggaley.
Dawa ya Truvada, ambayo ina mchanganyiko wa dawa
aina ya Tenovofir na Emtricitabine, imethibitishwa kuwa salama kwa
kupunguza makali ya VVU pia kuzuia maambukizi mapya. Dawa hizi
zinazotengenezwa nchini India, zimekuwa msaada mkubwa wa tiba kwenye
nchi zinazoendelea.