Papa Francis Kiongozi wa kanisa Katoliki
Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake hao 26
kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama
wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa
ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo.
Barua hiyo
inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na
kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa
akiunga mkono utamaduni wa useja,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa
huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa
akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu
katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita
Habari zaidi BBC Hapa>>
Habari zaidi BBC Hapa>>