Tunapenda kuwataka wanajamii kuwa makini sana na vitu ambavyo vinarushwa hewani na mitandao hiyo. Kwa kutumia uthibitisho wa utaalamu picha inayoonekana haina uhusiano wowote na msanii huyo. Kwa ufupi ni kwamba picha hiyo imetengenezwa kwa madhumuni ya kumchafua Madam huyo ambaye anawika kwenye tathnia ya filamu nchini.
Kwa kuthibitisha ukweli wa kutengenezwa kwa picha hiyo, mtaalamu wetu anatwambia tutazame kwa makini maeneo ya shingoni katika picha hiyo, Utaona cheni aliyovaa imegawanyika vipande viwili. Vilevile ukitazama vizuri nywele zake utaona kama vile zimechongwa kwa kisu. Kwa ufupi ni kwamba picha ya kichwa haiendani kabisa na picha ya chini (kiwiliwili).
Kwamtindo huu UTAMU WA RAHA inawataka wadau wa mitandao kuwa makini sana na vitu vinavyopostiwa na blogs. Wengine hufanya hivyo kwa madhumuni ya kumchafua mtu fulani ama kujitafutia umaarufu mwenyewe.