THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Hatua za kinidhamu zitachukuliwa
dhidi ya waliohusika katika udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne wa mwaka
2014 ambao wanafunzi 184 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu huo.
Kati ya wanafunzi waliofutiwa
matokeo 128 ni wa kujitegemea kutoka vituo viwili vya P2617 Kisesa mkoani
Mwanza na P4806 Ubago Visiwani Zanzibar na 56 ni watahiniwa kutoka shule
mbalimbali.
Akitangaza matokeo juzi jijini Dar
es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (Necta) Dk. Charles
Msonde, alisema wameiagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua za kinidhamu
waliohusika katika vituo hivyo kwa mujibu wa kanuni za utumishi.
“Lazma wahusika wachukuliwe hatua
kwani udanganyifu uliojitokeza ni karatasi moja ya kujibia mtihani kuandikwa na
watu watatu tofauti, jambo linaloonyesha hakukuwa na umakini,”
alisema
Katika matokeo hayo wanafunzi
196,805 (68.33%) wamefaulu kati ya watahiniwa wote 288,247
waliofanya mtihani huo huku kiwango cha ufaulu kikipanda kwa asilimia
10.08 ikilingnishwa wanafunzi 235,22 wailofaulu mwaka 2013
(58.25%).
Hata hivyo, kiwango hicho cha ufaulu
bado hakijafikia dhamira ya Serikali ya lengo la Matokeo Makubwa Sasa
(BRN) la kufikia aslimia 70, jambo linalohitaji nguvu zaidi kwa walimu,
wanafunzi na wadau wote wa elimu.
Dk. Msonde alisema matokeo ya mwaka
huu yanaonyesha bado ufaulu wa masomo mengi upo chini ya aslimia 50, Hisabati
(19.58), Biashara (34.29), Historia (37.41), Jiografia (37.96), Uraia (37.90),
Fizikia (46.71) na Kutunza Fedha (42.20).
CHANZO: NIPASHE