Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Kata ya Masekelo, Josephina
Kishiwa alisema alipata taarifa za tukio hilo juzi.
Shinyanga. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa
kushirikiana na wananchi wa Mtaa wa Masekelo, Manispaa ya Shinyanga wamelifukia
kaburi la Benadetha Steven (35) aliyezikwa na kifaranga tumboni lililofukuliwa
juzi na watu wasiojulikana kwa madai ya imani za kishirikina.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga, Musa Talib jana alilaani kitendo cha
kufukua kaburi hilo la Benadetha aliyefariki dunia Januari 3 mwaka huu.
Taibu alisema tukio hilo halivumiliki, hivyo aliwataka wananchi kushirikiana
na polisi kufanya uchunguzi.
Alisema wao pekee hawawezi kujua kinachofanyika, huku akiweka wazi kuwa
kaburi hilo halijatitia bali kuna watu wanaofanya mambo ya kishirikina.
“Mtu mwenye dini hawezi kufanya hivyo hizi ni imani za kishirikina haya
mambo ndiyo yanafanya watu waende kwa waganga wa kienyeji, hebu tujiulize mtu
ameshafariki dunia na kuzikwa, unakwenda kufukua kaburi lake unatafuta nini?
Tushirikiane kuwabaini waliofanya kitendo hiki,” alisema Taibu.
Taarifa za kufukuliwa kaburi hilo zilianza kusambaa juzi saa 1.00 usiku.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Kata ya Masekelo, Josephina Kishiwa alisema
alipata taarifa za tukio hilo juzi.
“Hili ni tukio la mara ya kwanza kutokea katika makaburi haya, hatujawahi
kukuta kaburi limefukuliwa...kwa kweli hiki kitendo kimetusikitisha sana,
tunaomba tu Serikali ifanye uchunguzi ili tujue chanzo cha tukio hil,” alisema
Kishiwa. Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mapinduzi Kata ya Ndala, Deo Masanja
alisema hawaamini kama fisi wanaweza kufukua kaburi hilo.
Alisema wakati wanamzika marehemu walichimba kaburi refu, lakini leo
wanashangaa kuona limekuwa fupi hadi jeneza na sanda vinaonekana. PITIA MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>