
MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi
Rwanda Nzovwe jijini Mbeya , Elika Mkubwa (8), amefariki dunia baada ya kubakwa
na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema
baada ya watu hao kufanya unyama huo, waliuweka mwili wa mtoto huyo katika
sinki la kuogea kwenye nyumba moja ambayo haijakamilika ujenzi wake. Pamoja na
hayo, alisema upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio
hilo.

Akizungumza eneo la tukio, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba,
Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi
kupitia kwa majirani zake.
Chanzo chetu kikizungumza na kiongozi wa
Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata
jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.

"Nilipota taarifa hiyo, niliongozana na majirani tukiwa na ndugu wa marehemu na kushuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea hukusehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya"

Mama mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema mtoto
huyo alitoweka nyumbani kwake January 7 mwaka huu baada ya kuaga anakwenda
kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji lililopo mbali kidogo na nyumbani
kwake. KUPITIA MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>