Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake amefariki dunia baada ya kugongwa na treni ns kuburuzwa umbali wa mita mia maeneo ya Kinguruwila mjini Morogoro.

Mwanahabari wetu akishuhudia tukio hili amesema kuwa viungo vya mwili wa mtu huyo ambavyo vimetapakaa umbali huo wa mita mia kama vile miguu, mikono, na kifua vimeokotwa lakini  kichwa hakikuweza kupatikana na hakijulikani kilipo.

Wananchi wa eneo hilo wamsema kuwa inawezekana mtu huyo alikuwa maelewa na kushindwa kuepukana na ajali hiyo.

Kamanda wa reli  Enginea Simon Chillery  akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea nachingwea amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo  na amesema mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake  anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40  na uchunguzi  wa tukio hilo unaendelea na kuwakumbusha wananchi kuheshimu sheria za reli kama ilivyo sheria za barabarani  kwa watembea kwa miguu  na wanaendesha vyombo vya moto wanapovuka reli
 
Top