
Mwanamke mmoja anayejihusisha na biashara ya kuuza mwili maarufu kama 'Changu' ama 'Popo' amezua kizaa zaa maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es salaam kwenye gest moja bubu baada ya kutaka kuzurumiwa na mteja wake ambaye amempatia huduma.
Songombingo hilo lilitokea baada ya jamaa mmoja (Fundi Magari) kumchukua mwanadada huyo kwa lengo la kujistarehesha baada ya mizunguuko ya mchana kutwa. Jamaa alikubaliana na changu huyo kupewa huduma kwa gharama ya shilingi 20,000 za kitanzania.
Kasheshe ikaanza baada ya jamaa kustareheshwa na Changu kisha kutaka kuingia mitini pasipo kulipia huduma hiyo kama ambavyo alikubalina kabla na muuzaji wake.
Changu alipoona amezidiwa nguvu na jamaa alikwenda mbele ya gari ya jamaa na kujilaza kwenye boneti ili kumzuia asiondoke. Vurugu hizo zilijaza watu jambo ambalo likamfanya jamaa kulipa deni lake haraka ili kuondokana na fedheha hiyo.
Baada ya kupewa chake Changu aliteremka kutoka kwenye boneti ya gari hiyo na kumuacha huru jamaa aondoke kisha na yeye akaingia kwenye mawindo yake.