Kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Matiko mkea amedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na baada ya siku kadhaa kupatikana akiwa amelala nyuma ya nyumba huku akiwa amefunikwa kwa nguo inayosadikiwa kuwa ni sanda.


Kitendo hicho cha kurejea kwa kijana Matiku katika hali isiyo ya kawaida imepelekea wananchi kupatwa na mshangao. Jambo lililosababisha wananchi kuvamia nyumba saba za watu waliokuwa wakishukiwa kuhusika na tukio hilo na kuzichoma moto.

matiku alieleza kuwa kabla ya kutoweka kwake alikuwa amekwenda kisimani ambako alisikia sauti mbili tofauti ya mwanamke na mwanaume zikimuita huku waitaji hawaonekani. Matiku aliposikia hivyo aliogopa na kusita kuitika ndipo akasikia sauti hizo zikimwambia kuwa alikuwa anaringia majini yake na kukwepa mitego yao mara kadhaa hivyo wakamueleza kuwa safari ile asingeweza kukwepa.

Baada ya maneno hayo Matiku ameeleza kuwa hakujitambua tena hadi pale alipojikuta akibanwa na kundi la watu kwa kumshika miguuni na mikononi na baada ya hapo hakuweza kujitambua tena hadi alipojikuta amelala akiwa amefunikwa kwa shuka nyeupe.
Kamanda wa polisi Serengeti amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Gati Kisibo amefariki dunia kutokana na kipigo hicho kutoka kwa wananchi.

Vilevile watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na ufanyaji wa vurugu na kuchoma nyumba pamoja na kusababisha kifo cha mtu mmoja.


 
Top