Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda
ya Dar es Salaam leo kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe
dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa
uanachama wake ndani ya chama hicho
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Akitangaza hatua hiyo ya kumvua uanachama,Lissu amesema kanuni na sharia za
chama hicho ziko wazi na zinaelekeza kuwa endapo mwanachama yeyote atakishtaki
chama hicho mahakamani na iwapo atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye
chama
HABARI ZAIDI ZA KISIASA BOFYA HAPA>>
HABARI ZAIDI ZA KISIASA BOFYA HAPA>>