Nabii kairuki ambaye kabla ya Kumpokea Yesu kristo aliwahiu
kuwa mwanachama wa Freemason, Amekanusha madai ya kwamba msanii mshuhuri wan
bongo flavor (Diamond) kuwa aliwahi kuwa
mwanachama wa chama hicho cha Freemason.
Kwakuthibitisha hayo Nabii Kairuki amezungumza na gazeti la
Visa na kusema kuwa mtu yoyote akiwa mwanachama wa chama hicho anakuwa na
alama, na hata kama akiacha alama hiyo haifutiki inaendelea kuwepo. Diamond
hana alama hiyo kwa mujibu wa Nabii huyo.
Kitu pekee ambacho anakitumia Diamond katika mafanikio yake
ni majini ya kichawi ambayo yapo saba. Nabii Kairuki anaendelea kusema kuwa
kuna utofauti kati ya Freemason na uchawi. Kwamujibu wa kimtazamo vitu hivi
viwili vinawiana kwasababu vyote vinamtumikia shetani. Utofauti wake ni kwamba
Uchawi unajiendesha kibinafsi wakati Freemason inajiendesha kichama na taasisi.
Kwa mujibu wa maelezo ya nabii Kairuki anadai kuwa anampenda
sana Diamond hivyo anamshauri awachane na majini hayo kisha amrudie Mungu. Na endapo
hatofanya hivyo mwisho wa msanii huyo unaweza kuwa wa majuto.
PICHA HII NI DIAMOND AKIWA NA TUZO YAKE
PICHA HII NI DIAMOND AKIWA NA TUZO YAKE