Mhudumu wa nyumba ya kupumzikia wageni ya kanisa la KKKT Dayosisi ya mashariki ya ziwa Victiria amejeruhiwa vibaya na Bomu lililokuwa limetegwa kwenye kreti la soda maeneo hayo.

Kulingana na chanzo cha habari hii, mhudumu wa Rest house hiyo Bi. Benaderta Alfred likumbwa na mkasa huwo alipokuwa akijaribu kukagua mfuko wa rambo mweusi uliokuwa umewekwa kwenye kreti ya soda iliyokuwepo kwenye nyumba hiyo karibu na eneo la kulia chakula.

Chanzo kimesema kuwa kitendo cha kufungua tu mfuko huwo bomu hilo lililipuka na kurusha misumari mingi sana hewani na kumjeruhi vibaya mhudumu huyo sehemu za miguuni.

Hadi sasa haifahamiki bomu hilo lilikuwa limetegwa kwa lengo la kumjeruhi mhudumu huyo ama mtu mwengine. Pia haieleweki kama mlengwa wa bomu hilo ndiye aliyejeruhiwa ama ni tofauti.



Inayo onekana kwenye picha hizi ni damu ya mhudumu aliyejeruhiwa na bomu hilo


Ukitazama kwa ukaribu zaidi utaona misumari iliyotoka kwenye bomu hilo lilipolipuka

 
Top